Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 27

KESHA LA ASUBUHI

JUMANNE, APRILI, 27, 2021
SOMO: UTHIBITISHO WA UJUMBE WETU 

Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe. 

1 Timotheo 4:1,2 



Nimeelekezwa kwamba Bwana kwa nguvu zake zisizo na kikomo aliutunza mkono wa kuume wa mjumbe Wake kwa zaidi ya nusu karne, ili kwamba ukweli uandikwe, kama alivyoniambia mimi niandike katika machapisho katika jarida na vitabu, kwanini? —kwa sababu kama yasingeandikwa hivyo, wakati waasisi wa imani watakapokuwa wamekufa, kutakuwa na watu wengi wapya katika imani, ambao wakati fulani wataukubali ujumbe wenye mawazo ya makosa na dhana za uwongo hatarishi kama ujumbe wa mafundisho ya kweli. 



Wakati fulani kile watu wanachotufundisha kama “nuru maalumu” kiuhalisia kina makosa ya kuhadaa ambayo kama gugu linalopandwa katikati ya ngano, litachanua na kuzaa mavuno maovu. Na makosa ya namna hii yataendelezwa na baadhi mpaka kufungwa kwa historia ya ulimwengu huu. 



Wapo baadhi ambao kwa kukubali nadharia zenye makosa, wanapambana kuziimarisha kwakukusanya semi kutoka katika maandiko yangu ya kweli ambayo wanayatumia yakiwa yametenganishwa kwenye muunganiko wake sahihi na kupotoshwa kwa kuunganishwa na makosa. Hiyo mbegu ya uzushi huchipua na kukua haraka na kuwa mti imara, unaozungukwa na miti mingi ya thamani ya ukweli, na kwa njia hii jitihada ya nguvu hufanyika kuthibitisha ukweli wa mti bandia. 



Ndivyo ulivyokuwa uzushi uliofundishwa katika Living Temple ( Kitabu kinachoelezea chembechembe za Mungu kuwa katika kila kiumbe, kilichochapwa na J. H. Kellog]. Makosa ya kistadi yaliyowekwa katika kitabu hiki yamezungukwa na kweli nzuri nyingi... ushawishi wa uongo wa Shetani unadhoofisha imani katika nguzo za kweli za imani zilizojengwa katika uthibitisho wa Biblia. Ukweli hudumishwa kwa maneno rahisi “Bwana asema hivi” Lakini kumekuwa na wimbi la makosa, na utumiaji wa maandiko kinyume na muunganiko wake wa asili ili kuthibitisha uongo, utakaowadanganya yamkini hata wateule... 



Hebu siku isipite na fursa za thamani zisipotee za kumtafuta Bwana kwa moyo wote, akili na roho yako yote. Kama hatutaukubali ukweli kwa kuupenda, tunaweza kuwa miongoni mwa wengi watakaoiona miujiza inayoletwa na Shetani katika siku hizi za mwisho na kuiamini. 



—Letter 136, April 27, 1906,, to Brethren Butler, Daniells, and Irwin.

Post a Comment

0 Comments