Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 23

KESHA LA ASUBUHI

Ijumaa 23/04/2021

*UTAZAME UPANDE WENYE MATUMAINI*

*Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.* Malaki 3:17

📜 Nina maneno ya kutia moyo kwa ajili yako. Yesu anakupenda. Aliyatoa maisha yake ya thamani ili usipotee, bali uwe na uzima wa milele. Basi yainue macho yako umtazame. Utazame upande wenye matumaini. Haitakufaidia kitu kuutazama upande usio na matumaini. Kuwa mvumilivu, hata iweje. Unaweza kupata nguvu kwa Yesu, kwani katika yeye ndimo ulimo ukamilifu. Wakati kukata tamaa kunapoisonga nafsi yako, endelea kumtazama Yesu. Iweke nafsi yako isiyo na msaada juu Yake. Anaishi siku zote akifanya upatanisho kwa ajili yako. Wewe ni wa thamani machoni pake. Yeye amtazamaye shomoro mdogo wa kahawia kwa upendo, anamtazama kwa upendo na huruma mtoto Wake aliyejaribiwa na kuteswa. 

📜 Mungu anataka kutuadibisha kwa furaha yetu ya sasa na kwa mema yetu ijayo. Baraka kubwa waliyonayo watoto wake ni nidhamu anayowapitisha ndani yake. Kamwe hatawaongoza vinginevyo kuliko vile ambavyo wangechagua kuongozwa kama wangeweza kuona mwisho tangu mwanzo na kutambua utukufu wa kusudi wanalolitimiza, kama watenda kazi pamoja Naye. 

📜 Mtendakazi wa kiungu anatumia muda mchache katika vitu visivyo na thamani. Hutumia muda mwingi kwa vito vya thamani, huing’arisha mithili ya jumba la kifalme, akizikata kingo zenye mikwaruzo. Mchakato huu ni wa kuumiza; Kristo hukata sehemu zilizozidi na kuliweka jiwe katika gurudumu la kung’arishia na kulikandamiza ili kwamba mikwaruzo yote iondolewe. Kisha akikishikilia kito katika nuru, ndani yake Bwana anaona akiakisiwa, naye hukitangaza kuwa cha thamani katika kibweta chake... 

📜 Kaka yangu mpendwa, daima mtazame Yesu na kuileta mbingu hapa chini maishani mwako. Njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba na tena imesonga, bali wote walio tayari watapita katika milango na kutembea katika njia nyembamba. Ili hatimaye tufike mbinguni, mbingu yetu ni lazima ianzie hapa chini. Kadri tunavyoileta mbingu katika maisha ya hapa ndivyo furaha yetu itakavyokuwa kubwa katika nyumba ya juu. 

🔘 *Hebu akili yako ikae katika wema wa Mungu, katika upendo mkuu kama alivyokupenda. Kama asingekupenda, asingemtoa Yesu kufa kwa ajili yako. Mikono Yake ya milele iko chini yako. Katika maumivu yako yote, Yeye anaumizwa. “ Uimara ni nguvu ambayo Mungu anaitoa kupitia kwa Mwanawe wa milele.”*

*TAFAKARI NJEMA SANA*👮‍♂️

Post a Comment

0 Comments