ZITTO KABWE; SIKU 100 ZA RAISI MWINYI ZIMELETA MATUMAINI MAKUBWA ZANZIBAR

• ZITTO; SIKU 100 ZA RAIS MWINYI ZIMELETA MATUMAINI ZANZIBAR

• Kwa mwendo huu alioanza nao, Rais @DrHmwinyi nina uhakika ndani ya miaka mitano, Zanzibar ile tuitakayo yenye utulivu, umoja na ushirikiano, itakuwa" Ndg. @zittokabwe, Kiongozi wa chama cha ACTwazalendo.

• Naamini kwa hatua za awali ambazo Rais @DrHmwinyi amechukua na nia njema zitaweza kuleta matunda yaliyotarajiwa ikiwa zitaendana na mabadiliko ya mifumo na ujenzi wa taasisi imara zitakazoendeshwa kiweledi na kufuata misingi ya uwajibikaji.

• Uamuzi wa haraka wa kuchunguza kuanguka kwa jengo la maajabu na kuwekwa wazi kwa muhtasari wa taarifa ya uchunguzi kulikofanywa na Waziri wa Utalii ni ishara ya mwenendo mpya wa uwajibikaji katika kushughulikia mambo ya umma.

• Tumefarijika kuona kuwa naye Rais @DrHmwinyi anakerwa na kutokuwapo kwa ufanisi wa kuridhisha katika maeneo ya bandari na ukusanyaji wa mapato.

• Wizara nyeti kama Utalii inayokusanya mapato kwa asilimia 82 ya fedha za kigeni za Zanzibar na asilimia 31 ya Pato la Taifa la Zanzibar, kupatiwa kijana tena wa kike, kwa Zanzibar hii ni hatua kubwa kwa Wanawake wa Zanzibar.

• Uteuzi wa vijana wengi, wa kike na wa kiume ni ishara nzuri sana kuhusu Zanzibar inayokuja. Kwa sababu vijana waliopewa majukumu mazito ndiyo viongozi wajao.

• Rais Mwinyi ameonesha utayari wa kushughulikia changamoto za Zanzibar za mpasuko wa siasa, umoja wa kitaifa, rushwa na ubadhirifu, changamoto katika utoaji wa huduma za kijamii, kukwamua changamoto zinazoikabili sekta binafsi, kukuza uchumi na kutatua tatizo la ajira.

• Ni vigumu kupima kazi za Rais katika siku 100 kwa sababu mara nyingi katika nchi zetu ambazo hazina muda wa mpito, siku hizo hutumika kuunda Serikali
Hata hivyo, baadhi ya matendo, maneno na haiba hutoa sura ya mwelekeo wa Serikali mpya.

ZITTO KABWE Kiongozi wa ACTwazalendo @zittokabwe 
#HABARI #BinagoUPDATES

No comments