MUKHSIN MAMBO AFARIKI DUNIA

TANZIA: Familia ya Marehemu Mzee Khalfan Hassan Mambo wa Mwanza, inasikitika kutangaza msiba wa ndugu yetu mpendwa  Bw. Mukhsin Mambo uliotokea Jumatatu, Tarehe 08/02/2021 nchini Marekani.

Kwa Uwezo wake Mwenyezi Mungu, tunatarajia marehemu kuzikwa Mwanza. 

Gharama za kufanikisha kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Marekani mpaka Tanzania ni kubwa, hivyo tunawaomba ndugu zetu Watanzania, Jamaa na Marafiki ushirikiano wenu katika kuchangia chochote kile kwa aliyejaaliwa ili kufanikisha kuusafirisha mwili wa marehemu hadi nyumbani kwa maziko.

Tunaomba michango itumwe kwenye Akaunti ya Benki ya CRDB kwa Pilly Nikita Mambo Account No. 0112022046800 au M-Pesa No. 0754431018 jina litakalojitokeza ni Pilly Nikita Mambo.

Ahsanteni sana na Mwenyezi Mungu (SWT) awabariki na awatie nguvu wote. Ameen na tuseme In Shaa Allah.

Innalilahi Wa Inna Ilayhi Rajiun - “Sisi wote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake Mwenyezi Tutarejea”

 R.I.P MUKHSINI MAMBO 
#BinagoUPDATES

No comments