Kikosi cha Namungo FC kimerejea hotelini usiku huu baada ya kushindwa kuondoka jijini Luanda, Angola kurejea Tanzania ikItumia kutwa nzima ya leo ikiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Luanda.
Namungo imeshindwa kusafiri kwa ndege ya kukodi baada ya wachezaji wake watatu na kiongozi mmoja waliokutwa na maambukizi ya virusi vya #Corona kutoruhusiwa na mamlaka kutoka karantini kujiunga na wenzao kwa ajili ya safari hiyo.
#NamungoFC
#BinagoUPDATES
0 Comments