Advertisement

Responsive Advertisement

#FAHAMU, HILI NDIO FUVU LA MTAKATIFU VALENTINE

Hili ndio fuvu la Mtakatifu Valentine .

Valentine alikuwa padre huko Italia mwanzoni mwa karne ya tatu. Alizaliwa mwaka 226 huko Terni Italia. Wakati huo Italia ilikuwa chini ya utawala wa Mfalme Claudio. Mfalme Claudio alikuwa anaamini kwamba vijana kushiriki tendo la ndoa ilikuwa inawafanya wawe dhaifu,kwa hiyo alipiga marufuku vijana kufunga ndoa. Kwa upande wake Padre Valentine aliendelea kufungisha ndoa kisiri siri. Habari hiyo ilipomfikia Mfalme, alikereka sana na kuamua Valentino akamatwe. Valentino alipokwenda kutembelea Roma alikamatwa na kutupwa gerezani. Tarehe 14 February mwaka 269, Valentino aliteswa na kisha kukatwa kichwa kwa amri ya Mfalme Claudio. Valentino alizikwa siku hiyo hiyo. Siku chache baadae wafuasi wake walikwenda kufukua kaburi lake na kurudisha mwili wake nyumbani. Kuanzia mwaka 496,  February 14 imekuwa ikiadhimishwa na Kanisa Katoliki kama siku ya Mtakatifu Valentine. Mabaki ya fuvu lake yamehifadhiwa katika Kanisa la Bikira Maria huko Roma Italia.
#BinagoUPDATES

Post a Comment

0 Comments