YANGA SC YAKAMILISHA USAJIRI WA FISTON ABDULAZACK RAIA WA BURUNDI

#MICHEZO YANGA YAMALIZANA NA MTAMBO WA MABAO

FISTON ABDULAZACK raia wa Burundi amemalizana na mabosi wa Yanga ili kuongeza makali kwenye safu yaushambuliaji.

Abdulazack ambae ni mshambuliaji yeye ni mshambuliaji ambae anacheza pia timu ya Taifa ya Burundi.

Nyota huyo alieletwa duniani September 5, 1993 ana umri wa miaka 27 anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa ndani ya Yanga kwenye usajiri wa dirisha dogo ikielezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili.

Walianzana Saido Ntibanzokiza kisha ikafuata Dickson Job na sasa ni zamu ya Abdulazack.

Nyot huyo pia amewahi kucheza ndani ya klabu ya ENPPI ya Misri ambapo jezi  yake namba anayoipenda ni 12.

Kwenye timu ya Taifa ya Burundi amecheza jumla ya mechi 49 tangu msimu wa 2009 na ametupia mabao 19.

Kwa mujibu wa Kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa Lengo kubwa la kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji nikufunga magoli zaidi.

#MICHEZO #BinagoUPDATES

No comments