WALIOKWENDA KUAPA HAWAKUWA NA BARAKA ZA CHAMA
"Waliokwenda kuapa, hawakua na baraka za chama. Hakuna kikao chochote cha maamuzi ndani ya chama kilichokaa kuwapitisha. Wamejikusanya wenyewe na kwenda bungeni. Kauli aliyotoa Halima kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe aliwapa baraka, huo ni uongo. Mbowe ameitisha kikao cha kamati kuu tarehe 27 Novemba ili kuwahoji kwanini wamekiuka utaratibu wa chama, pamoja na kuwachukulia hatua"
Uhakika nilio nao, hao 19 walioenda kuapa, walishirikiana na ofisi za NEC, pamoja na bunge kughushi nyaraka za chama, kujiteua bila kikao na kujipeleka kwenda kuapa. Huu ni USALITI mkubwa. Wote 19 wanafahamu orodha haiwezi kwenda NEC bila kupitishwa na Kamati kuu ikiwa na saini ya Katibu mkuu na mihuri ya chama. Na mimi sijasaini wala Manaibu wangu. Sasa NEC watueleze hiyo orodha waliyopewa ina saini ya nani?"
Kughushi ni jinai. Na ni jambo la aibu kama ofisi ya bunge na tume ya uchaguzi wanaweza kushirikiana na watu wachache ndani ya chama kufanya jinai ya kughushi kwa maslahi yao wenyewe. Naomba wanachama wa CHADEMA"
Mtoe maoni yenu ni hatua gani zichukuliwe dhidi ya akina Halima Mdee na wenzake. Maoni hayo yawasilishwe kabla ya kikao cha kamati kuu Novemba 27"
Ieleweke hawa sio wabunge wa Chadema. Ni wanachama wa Chadema walioamua kutumia mwavuli wa Chama kunajisi heshima zao na heshima ya chama chao. Chadema hatuwatambui. Ni wabunge wa viti maalumu kwa matakwa ya CCM, ni wabunge wa NEC na ni wabunge wa Spika Ndugai. Kwa ujumla CCM imeamua kujiundia kambi yake ya upinzani bungeni ili kuokoa Trilioni 2 za wafadhili zisipotee"
John John Mnyika, Katibu Mkuu wa CHADEMA, 25 Nov 2020, Kinondoni, Dar es salaam.
#BreakingNEWS #BinagoUPDATES
Post a Comment