AMKA NA BWANA LEO
#KESHA_LA_ASUBUHI
Ijumaa 13/11/2020
*TEMBEA NURUNI*
*Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze,Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako.* Zaburi 43:3
☄️ Katika siku hizi za hatari tunapaswa kuwa makini zaidi, tusiikatae miale ya nuru ambayo mbingu kwa rehema inatutumia, kwani ni katika hiyo ndipo tunapoweza kuitambua mitego ya adui.Tunahitaji nuru kutoka mbinguni kila saa, ili tuweze kutofautisha kati ya vitakatifu na vya kawaida, vya umilele na vya muda. Kama tutaachwa wenyewe, tutaboronga kila hatua; tutafuata mielekeo ya dunia, tutaepukana na kujikana nafsi na kuona hakuna haja ya kukesha kila saa na kuomba, na tutachukuliwa mateka na Shetani katika nia yake. Leo baadhi wapo hivyo. Wamekataa kupokea nuru ambayo Mungu amewatumia, hawatafahamu kitu kitakachowafanya wajikwae
☄️ Wote ambao majina yao hatimaye yatakuwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo,watapigana kiume vita vya Bwana. Watafanya kazi zaidi kwa dhati kubaini na kuyaweka mbali majaribu na kila kitu kiovu. Watahisi kwamba jicho la Mungu li juu yao na kwamba uadilifu thabiti unahitajika. Kama askari waaminifu wataidhibiti njia isipitike ili kwamba Shetani asije akawapita kwa hila, kama malaika wa nuru kuifanya kazi yake ya uuaji katikati yao...
🔘 *Wale Wenye mavazi meupe waliokizunguka kiti cha enzi cha Mungu, hawajumuishi wale ambao walikuwa wapenda wa anasa zaidi kuliko Mungu, na wale wanaochagua kufuata mwelekeo wa mambo kuliko kujizatiti kukabiliana na mawimbi ya upinzani. Wote wanaosalia kuwa safi na kutonajisiwa na roho na mivuto iliyoenea katika wakati huu watakumbana na migogoro mikali. Watapitia taabu kubwa; watayafua mavazi yao ya tabia na kuyafanya kuwa meupe katika damu ya Mwanakondoo. Hawa wataimba wimbo wa ushindi katika ufalme wa utukufu.*
Post a Comment