AMKA NA BWANA LEO

#KESHA_LA_ASUBUHI

ALHAMISI, NOVEMBA, 12, 2020

 *MUIMARIKE, MSITIKISIKE*

```Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.```

*1 Wakorintho 15:58*

✏️Wale wanaosimama katika kutetea heshima ya Mungu, na kudumisha usafi wa kweli kwa gharama iwayo yote, watakumbwa na majaribu ya kila namna, kama ilivyokuwa kwa Yesu katika jangwa la majaribu. Tabia ya kusalimu amri, kwa wale wasio na ujasiri wa kukemea maovu, bali wanakaa kimya wakati ambapo ushawishi wao unahitajika katika kuitetea haki dhidi ya msukumo wowote, wanaweza kuepuka huzuni kubwa na kuepuka mifadhaiko mingi na kupoteza thawabu kubwa kama siyo roho zao wenyewe.

✏️Wale walio katika mapatano na Mungu na kupitia imani katika Yeye, wanapokea nguvu kupingana na maovu na kusimama katika kutetea haki, mara zote watakutana na upinzani mkali na mara nyingi watasimama wenyewe. Lakini ushindi wa thamani utakuwa wao watakapomfanya Mungu kuwa tegemeo lao. Neema Yake itakuwa nguvu yao. Utambuzi wao wa wakimaadili utakuwa makini, angavu, na mwepesi kuhisi. Nguvu yao ya kimaadili itakuwa sawa kuhimili mivuto miovu. Uadilifu wao, wa tabia safi kama ule wa Musa.

✏️Itahitaji ujasiri wa kimaadili kuifanya kazi ya Mungu pasipo kuogopa. Wale wanaofanya hivi hawawezi kutoa upenyo wa kujipenda wenyewe, ubinafsi, tamaa ya makuu, kupenda starehe, au tamanio la kuepuka msalaba.... Je, tutii sauti ya Mungu au tusikilize sauti inayobembeleza ya muovu, na kufunikwa katika usingizi wa kufisha katika mkesha wenye uhalisia wa kuingia katika umilele?

🙇‍♂️*Mwokozi wetu anatamani kuwaokoa vijana.... anasubiria kuweka katika vichwa vyao taji ya uzima na kusikia sauti zao za furaha zikiungana katika kumpatia heshima na utukufu na enzi Mungu na Mwanakondoo katika wimbo wa ushindi utakaosikika na kusikika tena na tena katika nyua za mbinguni.*

*MUNGU AWABARIKI MNAPOTAFAKARI*

No comments