FUMBO LA UTAJIRI NA MAFANIKIO


 *FUMBO LA UTAJIRI NA MAFANIKIO*
Kwanza nianze kwa kukusalimu kupitia Jina La YESU, ninapokuletea ujumbe huu naomba ufahamu kuwa ninaposema kutajirika ni tofauti na kufanikiwa kwani; unaweza kuwa tajiri hujafanikiwa lakini pia unaweza ukawa umefanikiwa lakini sio tajiri au vyote ukawa navyo na pia vyote ukawa huna.

Watu wengi tunajitahidi Sana kujishughulisha pasipo mafanikio yoyote katika Yale tunayojibidisha, ndipo watu tunaingia kujaribu kila jambo liwezekanalo ili kutajirika, mfano wengine kuuza madawa ya kulevya, kujiuza, ujambazi, kwenda kwa waganga na hata kujaribu kufanya kila shughuli kwa ubashiri.

 *#Ndugu msomaji wa ujumbe huu,* naomba uelewe kuwa Asili ya Mafanikio na Utajiri hutoka kwa Mungu sio katika bidii zako binafsi, watu wengi tumekuwa tunajibisha lakini bidii hazijatusaidia, na hapo ndipo tunaanza kuona bidii tu sio jawabu la utajiri na mafanikio. Biblia imeweka bayana kuwa Mungu ndiye source (chanzo) cha Utajiri wetu na sio bidii zako,
 *Kumbukumbu la Torati 8:18 SRUV*
[18] Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

 *#Hata hivyo* , shida kubwa ya watu kutotajirika na kufanikiwa ni *KUTORIDHIKA na KIPATO KINACHOPATIKANA pamoja na KUKOSA UVUMILIVU.*
Hapa napenda uelewe kuwa; hakuna Mtu aliyeumbwa kusudi atajirike kwa kufanya kila jambo na likamfanikisha, kamwe huwezi wewe mwenyewe ukawa mfanya Biashara, wakati huohuo mkulima, mara mfugaji, na kadhalika  Aidha hapa ni Mungu akusaidie upate watu sahihi wenye kufungamanishwa na mafanikio au utajiri wa eneo hilo) Fikiria Kilichomkuta Labani kabla ya ujio wa Yakobo katika ufugaji wake, ile ni dhahiri kwamba eneo la Utajiri wake halikuwa yeye mwenyewe kufuga lakini yeye alikadhana na kufuga, na kufanikiwa au kutajirika kwake kulikuwa ni pale Yakobo alipokwenda kumsaidia eneo Hilo.
 *Mwanzo 30:30 KJV*
[30] Maana mali yako ilikuwa haba *kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, BWANA akakubariki kila nilikokwenda.* Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe?

 *#Kwa hakika Mungu* anafahamu kabisa ya kuwa wanadamu tunapenda kutajirika au Kufanikiwa lakini, kanuni ya Kutajirika au kufanikiwa imefungwa katika wakati, Biblia imeweka bayana kuwa kila jambo Lina wakati wake, haiwezekani ukadhani Utajiri na mafanikio huja kwa wakati uliojipangia wewe hili haliwezekani, Mungu ameweka fumbo na ili kulifumbua ni kwa njia ya kumwendea Mungu tena maana yeye ndiye mwenye Hilo fumbo, Ooh hallelujah.
 *Mhubiri  3:1,11 KJV*
[1] Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
[11] *Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake;* tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.

# *Lakini pia, Utajiri au Mafanikio huja hatua kwa hatua** , Jiulize kwanini Mungu aliumba Mbingu na Nchi pamoja na vyote vijazavyo akiwemo na Mwanadamu kwa siku 6, Je, Mungu angeshindwa kuumba vyote kwa siku moja? Jibu ni kwamba MUNGU ASINGESHINDWA, Lakini aliumba vile kusudi tufahamu ya kuwa *MUNGU NI MUNGU WA HATUA KWA HATUA,* Hata Utajiri na Mafanikio huja hatua kwa hatua.

 *Ayubu 8:7 KJV*
[7] Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, *Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.*
Hapa unaanza kuona ya kuwa Mungu anatambua kanuni ya kila mwanzo mdogo kuongezeka kwa ukubwa mwishoni, *huwezi kuanza Leo Leo Biashara ya nyanya leoleo ukawa na supermarket that's impossible,* hivyo unapopitia changamoto katika kile unachojibidisha haimaanishi Utajiri au Mafanikio yako hayapo katika unachojibidisha, kwani inawezekana unapitishwa darasa la Uvumilivu na kukomazwa zaidi katika eneo Hilo.
 *Mhubiri 9:11 KJV*
[11] Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

 *#Mwisho, Huwezi* kutajirika au kufanikiwa Bila ya kujua wewe ni NANI? na ULIUMBWA KWAAJILI YA NINI? Ikumbukwe kila Binadamu amefanywa na Mungu kwa upekee wa Aina yake, na kila mtu kuna kitu amewekewa akifanye kusudi kimsaidie yeye na Kumuunganisha Karibu na Mungu wake, Ndio maana sio wote tunaweza kuwa na kazi moja duniani, Uwepo wa shughuli mbalimbali duniani ni mojawapo wa kusudi la Mungu kwaajili ya *UENDELEVU WA UUMBAJI WA MUNGU,* Mungu alipomuumba Mwanadamu aliagiza kuongezeka na kuijaza Nchi na hapa sio kwa kuzaa watoto tu bali pia kupitia MAARIFA na UJUZI tuliopewa na Mungu na kujifunza kupitia mazingira yetu tunayoyaishi, ndio maana Mungu hakuwahi kujenga ghorofa lakini binadamu amejenga ghorofa yote hii ni kusudi kuijaza Nchi.
 *Mwanzo 1:28 KJV*
[28] Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Kujijua wewe ni Nani, na uliumbwa kwaajili ya nini ni FUNGUO TOSHA itakayokusaidia kukuletea UTAJIRI MKUBWA AU MAFANIKIO kwani *MUNGU HUFUNGAMANISHA PACKAGE YA MAFANIKIO NA UTAJIRI WAKO KUPITIA KUSUDI LAKO DUNIANI.*

HIvyo kama kuna jambo watu tumefeli, ni kuomba utajiri na Mafanikio Bila ya kuomba kujijua wewe na kusudi la Mungu juu yako, Hebu jiulize umewahi kumuuliza Mungu ufanye nini kusudi ufanikiwe au Utajirike? au ndio unajaribu kupapasapapasa ukijua kwa namna Fulani ndio utatoka kimaisha?
LEO NAOMBA UELEWE KUWA MUNGU UKIMUULIZA MASWALI YA KUSUDI LAKE JUU YAKO NA UKIFUNGAMANA NALO TAYARI UTAJIRI NA MAFANIKIO VITAKUFUATA, na UKIJUA KUSUDI MUULIZE UJISHUGHULISHE NA NINI, UTAPATA KUJIBIWA NA MIMI NAKUOMBEA MUNGU AKUJIBU NA KUKUFUNGUA NA FUMBO LA UTAJIRI NA MAFANIKIO KWA JINA LA YESU.

Wasiliana nami kupitia;
Email: elishasaimoney@gmail.com
0743839720 WhatsApp number
0765830426
0657076518 SMS & CALLS
*Shepherdelisha_International_Ministry*

No comments