Kanisani la kiadiventista wasabato lazindua chuo kikuu cha afya Rwanda

Rais wa Rwanda Mh,Paul Kagame akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Pr.Teddy Wilson kwa pamoja wakisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi,mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa chuo hicho leo mjini Kigali,nchini Rwanda.

Mandhari ya chuo kikuu cha afya nchini Rwanda kinavyoonekana mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo mjini Kigali,nchini humo. Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Pr.Teddy Wilson amezindua chuo kikuu cha Afya nchini Rwanda kwa lengo la kutoa fursa ya elimu ya afya kwa wanafunzi wa Mashariki ya kati ya Afrika. Hafla fupi ya uzinduzi wa chuo hicho cha afya kinachomilikiwa na kanisa la Waadventista wasabato mashariki kati mwa Afrika, limefanyika leo mjini Kigali ambapo Teddy Wilson amesema elimu bora siyo jengo bali ni huduma bora inayotolewa ndani ya majengo hayo huku akisema chuo hicho licha ya kutoa elimu ya afya inatoa huduma ya kiroho.

No comments