Haya ndio maneno ya Askofu Malasusa juu ya Marehemu Balozi Kaduma

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Malasusa amesema watamuenzi mwanasiasa wa zamani nchini humo, Balozi Ibrahim Kaduma kutokana na mchango wake kwa kanisa hilo.

Amesema Balozi Kaduma ndiye aliyetoa kiwanja cha ujenzi wa kanisa hilo, Makongo Juu Dar es Salaam na kusimamia kamati ya ujenzi ya kanisa hilo.Awali, Askofu wa kanisa la AICT, Dayosisi ya Pwani, Charles Salala aliwataka Wakristo kutunza muda kwa kufanya mema kwa sababu ukipita haurejei.

Balozi Kaduma anasafirishwa kesho asubuhi Jumatano Septemba 4,2019 kwenda Kibena mkoani Njombe na atazikwa nyumbani kwake Alhamisi ya Septemba 5,2019.

No comments