Askofu Ruwa'ichi apata nafuu

Askofu Ruwa’ichi alipata ugonjwa wa kiharusi Septemba 8 mkoani Kilimanjaro na alipata matibabu ya awali Hospitali ya Rufaa ya Kilimanjaro (KCMC) na baadaye kuhamishiwa Moi.

Jopo la madaktari bingwa na wauguzi wa Moi walimfanyia upasuaji mkubwa kwa muda wa saa 3.

Kwa mara ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji huo juzi alishiriki ibada katika wodi ya hospitali hiyo akiwa amekaa, jambo ambalo limeleta matumaini kwa madaktari wanaofuatilia afya yake.

No comments