Papa Alaani Shambulio la wahamiaji Libya

Vatican. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amelaani shambulizi la anga lililosababisha vifo vya zaidi ya wahamiaji 50 nchini Libya.

Shambulizi hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita linadaiwa kufanywa katika kambi ya wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali ikiwamo bara la Afrika.Akizungumza katika ibada ya Jumapili, Papa Francis alisema kuwa jamii ya kimataifa haiwezi kuvumilia matukio mabaya kama hayo.

Akiwahutubia waumini katika Uwanja wa Mtakatifu Peter, Papa Francis aliowaombea waathiriwa wa tukio hilo na kutoa wito kwa Serikali ya Libya kuhakikisha inachukua hatua haraka ili kuwaondoa wahamiaji katika mazingira ya hatari.

Aidha, Papa Francis pia aliwaomba waumini kushirikiana naye katika muda wa ukimya kuwakumbuka waathiriwa wa mauaji ya kiholela ya hivi karibu nchini Afghanistan, Mali, Burkina Faso na Niger.

No comments