Mchungaji Natasha afichua siri ya historia yake ya mapenzi

Mchungaji Lucy Natasha ambaye amehamasisha na kuimarisha maisha ya watu wengi nchini Kenya na pia Kimataifa amebaini wazi sifa za mchumba anayemtauta.

Mhubiri maarufu wa jiji amesifiwa kote kwa kuwa mchungaji mrembo kama tausi nchini na mara kwa mara wafuasi wake wengi hujiuliza kwa nini mwanamke aliye na uzuri, akili, na uaminifu huo bado hana mchumba?
Lucy alifichua kuwa kwake, kutafuta mtu sahihi ni muhimu kwa maisha yake ya mapenzi na aneweka Mungu mbele. Pia alielezea jnsi uhusiano wake wa awali na jinsi haikufanikiwa.

“Nilikuwa kwa mapenzi ambayo haikufanikiwa, ni kwa sababu inachukua muda mrefu kabla ya kupata mtu aneyekufaa.”
Katika maneno yake na kunukuu Biblia, anaamini kweli kwamba kila mtu ana wa kwake. Kwa hiyo licha ya changamoto alizopitia, hajakata tamaa na ana matumaini kuwa atakuja kuwa na familia siku za usoni.
Kwa kweli nataka kumpata mtu aneyenifaa, sitaki kitu cha kuombea, nataka mtu wa kuomba nami.”
Lakini ni sifa gani mchungaji angependa kwa mwaaume mwenye bahati nasibu? Anataka mtu anayewogopa Mungu, mwenye anavutiwa kwake na pia aliye na malengo na maadili.

Na kwa kuongezea, anataka wana wawili kwenye familia yake.

No comments