Askofu amfungia mmama moja huko Mombasa kwa kosa la kuchelewa kanisani

Mama mmoja mjini Mombasa aliishtua mahakama baada ya kuelezea jinsi askofu mmoja amekuwa akimtesa huku akimfungia katika chumba cha kulala kwa miezi mitatu.

Katika kesi iliyoskizwa Jumanne, Julai 9, korti ilielezwa jinsi Evans Manyenyo alimfungia Hellen Chelanga kutoka na hulka ya mama huyo kuchelwa nje akiwa anawatembelea wagonjwa.Chelanga alielezea mahakama vile vie kwamba bwanake, ambaye ni mtumishi wa Mungu tajika, aliudhika sana baada ya yeye kujiunga na kundi moja la kuisaidia jamii na akaahidi kumuonyesha kilicho mtoa kanga manyoya.

"Bwanangu alisema atanifunza adabu. Hapo ndipo alianza kunifungia ndani ya chumba chetu cha kulala kuanzia asubuhi mpaka jioni. Alinifungia na kunipa mkebe wa kuendea haja. Alikuwa akinifungulia usiku tu baada ya yeye kurudi nyumbani," mama huyo alisimulia.Huku washirika wa kanisa wakitoa ushahidi wao mahakamani mbele ya jaji Joshua Nyarike, mshirika Ephraim Amugune alisema kanisa lilishikwa na wasiwasi baada ya Chelanga, mke wake askofu wao, kuwacha kufika kanisani.

"Kila wakati tukimuuliza askofu, alikuwa akitueleza kuwa mke wake ni mgonjwa. Hata hivyo, mkewe baadaye aligundua kuwa bwanake alikuwa ameoa msichana fulani kutoka kanisa hiyo," aliambia mahakama.

No comments