Simba wana faida ya kucheza nyumbani ila sio mchezo rahisi


 Ameandika @mkazuzutza 


Kauli ya Simba sc kuelekea mechi dhidi ya Wydad Casablanca pale Benjamin Mkapa mchezo ambao Simba anahitaji zaidi alama tatu na Wydad anahitaji zaidi alama.


Kwa namna kundi lilivyo mpaka sasa Asec Mimosas inaoekana ndo timu yenye uhakika wa kutinga hatua inayofata huku Wydad Casablanca na Simba sc zikionekana moja kati yao inaweza kusonga mbele huku Jwaneng Galaxy ikipewa nafasi ndogo.


Ugumu wa mechi unakuja kutokana na msimamo wa kundi ulivyo, Simba wana alama mbili wanaburuza mkia, wanahitaji alama tatu muhimu ili kufikisha alama tano huku wakisubiri Jwaneng Galaxy pia waje kwa Mkapa waweze kuchukua alama tatu nyingine ili wafikishe alama nane wakienda kucheza dhidi ya Asec Mimosas wakatafute alama tatu au moja which is possible.


Lakini pia hesabu za Wydad ni kukusanya alama tatu kwa Mkapa wajihakikishie kuwa na alama sita huku wakisubiri mechi mbili moja dhidi ya Asec Mimosas na nyingine dhidi ya Jwaneng Galaxy kule Botswana.


Kwahiyo ni mechi yenye hadhi ya fainali kutokana na uhitaji wa alama tatu kwa kila timu ndiomaana joto na presha ya mchezo imekuwa kubwa kuliko kawaida.


Simba ina kocha mpya Benchikha na tayari tumeanza kuona mabadiliko kwa wachezaji na namna timu inacheza, lakini Wydad Casablanca tayari imeachana na kocha wao hivyo kesho kweye touchline kutakuwa na mwalimu wao aliyepewa majukumu kipindi hiki.

No comments