KIPORO CHA Simba vs Azam ni baada ya AFCON 2024
𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔, 𝗔𝗭𝗔𝗠 𝗕𝗔𝗔𝗗𝗔 𝗬𝗔 𝗔𝗙𝗖𝗢𝗡
Kile kiporo cha Simba na Azam kilichotarajiwa kupigwa Januari Mosi hakitapigwa tena sambamba na mechi nyingine za viporo kutokana na Bodi ya Ligi (TPLB) kuweka bayana kuwa ni ngumu kucheza kwa kubanwa na kalenda ya michuano tofauti ikiwamo fainali za AFCON 2023.
.
Michuano hiyo itapigwa kati ya Januari 13 hadi Februari 11, 2024 nchini Ivory Coast, na Tanzania ni miongoni mwa timu shiriki, hivyo kufanya baadhi ya mechi za Ligi Kuu kuvurugwa kwa sasa ikiwamo hiyo ya Simba na Azam na ile ya Januari 4 kati ya Simba dhidi ya Geita Gold, sambamba na kiporo cha Yanga na Dodoma Jiji.
.
Simba na Yanga kwa sasa zinacheza mechi za viporo, Simba ikianza dhidi ya Kagera Sugar juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, KMC utachezwa Desemba 23, Mashujaa umepangwa kuchezwa Desemba 26 ugenini Uwanja wa Lake Tanganyika na Tabora United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ni Desemba 29. Hata hivyo, mechi na Tabora United nayo haina uhakika kama itachezwa kwani tayari mashindano ya Kombe la Mapinduzi yatakuwa yameanza na Simba inashiriki. Mashindano hayo yanaanza Desemba 28 Unguja, Zanzibar.
Kwa upande wa Yanga, mechi ya Desemba 29 dhidi ya Mashujaa nayo iko kwenye hatihati kwani Kombe la Mapinduzi litakuwa limeanza. Yanga baada ya mechi ya jana dhidi ya Mtibwa, itakuwa na mechi nyingine dhidi ya Tabora United itakayochezwa Desemba 22 na ya Kagera Sugar itakuwa Desemba 26 zote zikichezwa ugenini.
.
Kutokana na kuwepo kwa mwingiliano wa ratiba ya Ligi Kuu na Kombe la Mapinduzi, TPLB imesogeza mbele mechi zote za Januari na sasa zitachezwa baada ya michuano ya Afcon kumalizika Februari.
Post a Comment