Tumeongea na Adebayor, Morrison hakuwa mtukutu Yanga.

⚽ Klabu ya Simba 🦁 jana Dhidi ya Kagera Sugar 🇹🇿 wamefunga goli la Offside, goli la pili lilikuwa ni la Offside, goli la john bocco 🇹🇿 lilikuwa ni Offside, mimi nilidhani ni beki wa Kagera kumbe ni John Bocco, Simba inafunga magoli mengi ya Offside" - Makamu Mwenyekiti wa Yanga Sc, Frederick Mwakalebela

"Simba sio mpinzani wa kweli, simba ana chupli chupli nyingi, majuzi anaifunga Ruvu Shooting golikipa wa Ruvu anafurahia kufungwa na Simba, tena hadi na party amefanya nyumbani, Simba kama ni mshindani wa kweli mbona haifungi yanga" -

⚽GEORGE MPORE 🇹🇿 MCHEZAJI WA KAWAIDA SANA.

-Mshambuliaji George Mpole 🇹🇿 ni Mchezaji wa kawaida sana, kuongoza au kufunga magoli kwenye ligi kwa sasa sio swala kubwa, siwezi kusema ni mzuri kiasi hicho, ni wa kawaida sana" - 

⚽BERNARD MORISSON HAKUWA MTUKUTU YANGA 🗣 

-Bernard Morrison 🇬🇭 alipokuwa yanga hakuwahi kuonesha utovu wa nidhamu, Swala la Morisson hatuwezi kuliongelea sasa hivi, lakini ni mchezaji ambaye kila klabu ingependa kuwa nae, ni mchezaji mzuri ila nidhamu yake tu ndiyo shida" - 

⚽ Yanga tumeongea na Victorien Adebayor, yule bado sio mchezaji wa Simba, kama wameshamalizana nae waoneshe basi mkataba wa awali, hata sisi tunaweza kumchukua" 
 Ameongea 🗣➡️ Frederick Mwakalebela
Tv3 Tanzania


No comments