Manara anaiponda Simba SC kwa mara nyingine

Ameandika Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Haji Manara.

"Mwaka 1987 Makolo ilibaki kidogo washuke daraja, mechi ya Mwisho ikabidi ifanyike Bonge la Chupli ili kuwanusuru, Match fixing ya kufa mtu, Eti wakatoka sare 5-5 na Tukuyu Stars, GD ikawanusuru. 

1988, Kwa huruma ya Yanga katika mechi ya mwisho ya msimu, ikakubali kupoteza kirahisi kwa kufungwa 2-1 na Makolo, Goli lao la ajabu ajabu toka kwa John Makelele.

Kiufupi Yanga alikosa ubingwa wa Msimu katika mechi ya mwisho ili kumnusuru mtani wake asishuke daraja, nakumbuka kipa wa Yanga alikuwa Marehemu Sahau Kambi....
Wananchi waliachia ubingwa ili Makolo tuendelee kuwa nao Ligi kuu, msimu huo Bingwa alichukua Coastal Union. 
1989, huu pia ulikuwa mwaka wao wa Shetani, Chupu Chupu kuteremka daraja, Once again Yanga ikawanusuru Kwa sare pacha katika mechi ya mwisho 0-0, kina Abedi Mziba na Joseph Machela wanaingia hadi kwenye Sita wanapaisha,ili tu kuwanusuru Makolo, uzuri msimu huo tayari Wananchi walishatwaa ubingwa kabla ya mechi ya mwisho kwenda kucheza na FC Makolo. 

Yanga hata iwe mbovu vipi haijawahi kupigania kushuka daraja hata siku moja, wenzetu mara kadhaa Yanga imeshawanusuru, ni vile Basi tu, Makolo hawana Shukran, walitakiwa kila Asubuhi wanatuamkia, kukosa Yanga, sasa hivi wangekuwa wanacheza na DTB na Kitayosa huko, Gastadialo. 

Nimeona niwajuze haya ili mpate kujua tulipotoka, na muweke akili zenu barabara, Msimu huu mkizubaa mtashuka kweli, Ndegelec.

Mkinuna natuma Mapato ya Tarehe 30 April 🤪"

No comments