UMMY MWALIMU AKABIDHI PIKIPIKI 74 KWA MAKATIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu leo Septemba 7, 2021 amekabidhi jumla ya pikipiki 74 kwa Makatibu Wasaidizi Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu zenye thamani ya shilingi milioni 218.
Akikabidhi pikipiki hizo Waziri Ummy amesema lengo ni kuboresha utendaji kazi wa tume hasa katika kutembelea walimu ili kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za kiutumishi zinazowakabili.
Akiongea mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Waziri Ummy amewataka Makatibu Wasaidizi wa Tume kuhakikisha vitendea kazi hivyo vinatumika kwa masuala ya utekelezaji wa majukumu ya kila siku zisigeuzwe kuwa bodaboda.
Amewataka Makatibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu kuhakikisha wanasimamia kwa weledi kada ya waalimu kwa kuwa ndio wenye jukumu kubwa la kuandaa taifa letu ili liweze kuendana na kufanikisha malengo yake katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha, amewasisitiza Tume ya Utumishi wa Walimu kuendelea kusimamia maadili na wasisite kuwachukulia hatua walimu wanaokiuka maadili hasa wale walimu wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.
“Simamieni maadili na nidhamu hatua zichukuliwe kama kuna maadili yamekosekana katika utumishi wa Umma hasa kwenye kada ya ualimu ambapo Taifa linategemea sababu mmeaminiwa katika kutenda haki kwa wananchi” amesema Ummy
Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa wanawajibu wakuhakikisha wanawasikiliza, kwa karibu na kutatua changamoto zao kwa wakati kwa kuwa wameaminiwa kuwasimamia kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ya utumishi wa Umma

Post a Comment