Advertisement

Responsive Advertisement

DIDIER GOMES DA ROSA ABADILI MBINU SIMBA SC

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amelazimika kubadili mfumo wake katika kikosi chake ili kutoa nafasi kwa majembe mapya yaliyoingia kikosini ambao yameonekana kumpasua kichwa jinsi ya kuwatumia.

Awali Gomes alikuwa akitumia mfumo wa 4-2-3-1,
4-3-3 au 4-4-2, lakinio kwa sasa ameutambulisha
mpya wa 3-5-2 uliokuwa awali ukitumiwa na mtangulizi wake, Svena Vanderbroeck aluiyepo FAR Rabat ya Morocco kwa sasa.

Mfumo huo mpya wa 3-5-2, ambao Gomes
ameutambulisha ulikuwa ukitumika pia zaidi na
aliyekuwa kocha wa Simba, Mfaransa Pierre
Lechantre ambaye alifanikiwa kutwaa ubingwa wa
Ligi Kuu Bara.

Mfumo huo unatumia mabeki asilia wa kati watatu, viungo watano ambao asilia wanakuwa watatu pamoja na mabeki wa pembeni wawili wanaunda eneo la kiungo kisha washambuliaji asilia wanakuwa wawili.

Kwa sasa ameamua kuutumia mfumo wa Mfaransa mwenzake huyo kutokana na ubora ambao wamekuwa wakionyesha mabeki wa kati, Hennock Inonga, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Kennedy Juma.

Gomes amelazimika kufanya hivyo, kutokana na
wachezaji hao na wale walioingia kikosini kwa
msimu huu kuonekana kuwa moto na kumpa wakati mgumu jinsi ya kuwatumia.

(Via;MO)

Post a Comment

0 Comments