Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 21/09/2021

*KESHA LA ASUBUHI* 

 *Jumanne, Septemba 21,2021* 

 *MUNGU NI NAFSI* 

" _Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyodhahiri_ ."
Waebrania 11:3

▶️ Ulimwengu wote wa asili unatoa ushahidi wa kazi za Mungu aliye hai. Asili ni kitabu chetu cha kujifunzia,tulichopewa na Mungu,Muumbaji wa vitu vyote.Vitu hivi vya asili havipaswi kuitwa Mungu.Hivi ni udhihirisho wa tabia ya Mungu,bali vyenyewe si Mungu.Kwa vitu alivyoviumba,tunaweza  kumfahamu Mungu, na Upendo wake,nguvu Zake, na utukufu wake,lakini kuna hatari kubwa ya watu kuiabudu asili kama Mungu.

▶️ Ujuzi wa kisanii wa wanadamu hutoa sampuli za kupendeza sana za kazi ustadi, zikidhihirisha vitu ambavyo hupendeza macho, na vitu hivi vinatupa wazo fulani kuhusu mbuni, lakini kitu kilichotengezwa si mtu yule aliyebuni vitu hivyo vyenye kuthaminiwa sana. Ndivyo ilivyo kwa asili. Uweza wa Bwana unadhihirishwa daima kama uweza utendao miujiza, ili familia ya wanadamu waweze kuona kutokuwa na kikomo juu ya ng'ambo ya pili ya vitu vilivyotengezwa, ili wajue kwamba Yeye aliyeumba nafsi kama kwa mwanadamu, ameumba pia vizuri vyote vya ulimwengu wa asili.
▶️Kuna hoja nyingi katika ulimwengu wetu leo kuhusu Muumbaji kutokuwa Mungu binafsi. Mungu ni nafsi na mwanadamu aliumbwa kwa mfano wake. Baada ya Mungu kumuumba mwanadamu kwa mfano wake,umbo hilo lilikuwa kamili katika Mpangilio wake wote, lakini halikuwa na nguvu ya uhai.Ndipo Mungu binafsi,mwenye uhai wake mwenyewe alipuliza katika umbo lile pumzi ya uhai na mwanadamu akawa kiumbe hai, anayepumua, mwenye akili. Sehemu zote za mashine za wanadamu ziliwekwa katika Mwendo.Moyo,mishipa ya ateri, mishipa ya vena, ulimi,mikono, miguu,utambuzi wa akili milango ya fahamu, viliwekwa chini ya sheria ya asili.Hapo ndipo mtu huyo akawa nafsi hai.

▶️ Kupitia kwa Yesu Kristo, 
Mungu - si manukato, si kitu kisichoshikika,lakini Mungu mwenye nafsi - alimuumba mwanadamu, na akamjaalia akili na nguvu....
▶️ *Bwana ni Mungu aliye hai, aliye na  nafsi. Mwokozi mwenye sifa alikuja katika Ulimwengu wetu ili kufanya kuwa bure minenguo yote ya kuhadaa na kugeukageuka kama nyoka wa shetani* .

*MUNGU AKUBARIKI SANA👮‍♂️*

Post a Comment

0 Comments