Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 20/09/2021


*KESHA LA ASUBUHI* 
Jumatatu: 20/09/2021

 *SOMO: KRISTO NDIYE NJIA* 

" _Filipo akamwambia, Bwana,utuonyeshe  Baba,yatutosha.Yesu akamwambia,Mimi nimekuwepo pamoja  nanyi siku hizi zote, Wewe usinijue,Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba."
_ Yohana 14:8,9

▶️ Hatuwezi kumwona Mungu kwa kuchunguza.Lakini amejidhihirisha mwenyewe katika uthibitisho  wa sifa zilizobainishwa na Kristo, ambaye ndiye mng'aro wa utukufu wa Baba, na picha halisi ya nafsi yake. Ikiwa tunataka kumjua Mungu,lazima tuwe kama Kristo....

▶️ Yeye ambaye hatafuti kila siku kuwa kama Kristo,hawezi kujua tabia ya Mungu.Kuishi maisha safi kupitia imani katika Kristo kama Mwokozi binafsi humleta Muumini katika Ufahamu safi na wajuu zaidi wa Mungu.Hakuna mtu ambaye tabia yake si nzuri na iliyo kama ya Kristo anayeweza kumwelezea Mungu kwa nuru sahihi.Anaweza Kumhubiri Kristo, Lakini hawaoneshi wasikilizaji wake kwamba Kristo ni mgeni wa kudumu katika Moyo wake....

▶️ Wale ambao ni washiriki wa upendo wa Kristo kupitia katika kuupokea ukweli watatoa ushahidi wa hili kwa kufanya juhudi zaidi,za kujitolea kutoa ujumbe wa upendo wa Mungu kwa wale walio katika makosa. Kwa hivyo wanakuwa watenda kazi pamoja na Kristo.Upendo kwa Mungu na wa mtu na mwenzake unaunganisha roho kwa Kristo. Kwa viungo vya dhahabu vya Upendo. Nafsi imefungwa pamoja naye Fkatika Umoja uliotakaswa,ulioinuliwa.

▶️ Utakaso wa Kweli unawaunganisha waumini kwa Kristo na wao kwa wao katika vifungo vya huruma.Muungano huu husababisha kutiririka daima ndani ya moyo mikondo tele ya Upendo kama wa Kristo,ambayo hutiririka tena kwa Upendo wa kila mtu na mwenzake.

▶️ Sifa ambazo ni muhimu kwa wote kumiliki ni zile zilizoashiria ukamilifu wa tabia ya Kristo - Upendo wake,Uvumilivu wake,Ukarimu, na wema wake...

▶️ *Ni udanganyifu Mkubwa na Mbaya kabisa kudhani kwamba mtu anaweza kuwa na imani hadi kupata uzima wa milele, bila kuwa na upendo kama wa Kristo kwa ndugu zake. Yeye ampendaye Mungu na jirani yake amejazwa nuru na upendo. Mungu yuko 

Post a Comment

0 Comments