*KESHA LA ASUBUHI.*
*Jumapili, 19/09/2021.*
*JINSI YA KUWA NA MBINGU HAPA.*
*"Waitamani nchi iliyo bora,yaani ya mbinguni." Waebrania 11:16.*
▶️ Tunataka kujitahidi kwa Nguvu zote ambazo Mungu ametupa kuyafunua Maandiko kwa wale ambao wako gizani. Kuna furaha, matumaini, na amani kwa wanaokata tamaa. Hatuwezi kuthubutu kutoa uwezo wetu tuliopewa na Mungu na kuutenga kwa ajili ya vitu vya kawaida vya dunia hii. Tunaitaka imani ile ambayo itashika kwa Nguvu ahadi iliyowekwa mbele yetu katika injili. Itakuwaje tukipoteza nafsi yetu? Ingekuwa bora kwetu kama kamwe tusingezaliwa. Nafsi moja ina thamani zaidi ya dhahabu na fedha zote zinazoweza kuwekwa rundo juu ya dunia hii...
▶️ Tunataka kukuza imani iliyo hai kwa Mungu. Tunataka macho yetu yageuke mbali na vivutio vya dunia hii na kulenga mbinguni na kwa vitu vya mbinguni. Hatutaki dunia iingilie kati yetu na Mungu, bali tunataka kujaza jicho kwa utukufu wa Mungu. Tunazungumza juu ya mbingu na baraka zake, na itakuwa hasara kubwa kuipoteza . Sawa basi kama ni ya kumpendeza kiasi hicho, ya kutamanika kiasi hicho, mwilete katika maisha haya, mwilete katika familia zenu na mwaelimishe watoto wenu wasiishi kwa ajili ya ulimwengu huu bali kwa ajili ya maisha ya baadaye, ya milele.....
▶️ Unaweza kuwa na mbingu ndogo hapa chini, iwapo tu utakaza jicho lako kwa Mungu -sio kumtazama kristo nusu wakati na kwa nusu nyingine kuutazama ulimwengu. Unapoishi kwa ajili ya Mungu ataweka mkono wake wa milele chini yako ,na ndipo anaposema, "nira yangu ni laini na mzigo wangu mwepesi" (Mathayo 11:30). Je, unaliamini hilo? Ninaweza kushuhudia kuwa hivi ndivyo ilivyo. Kwa uzoefu wangu wa zamani ninaweza kushuhudia kwamba nisingependa kupungukiwa na jaribio hata moja, kupungukiwa hata na huzuni moja, kwani paulo anasema "Dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanya utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana" (2 wakorintho 4:17,18)
▶️ *Tunataka kuangalia vitu vyenye manufaa ya milele ,ili tupate kufikiri kwa makini juu ya matumizi ambayo tumefanya kwa kutumia uwezo wetu wa kufikiri kama tumejaribu kuziimarisha kwa vitu visivyofaa ambavyo hatutaweza kuvichukua pale tutakaponyakuliwa kwenda kumlaki kristo hewani.... Tunataka tufae ili tupate haki tele ya kuingia katika mji wa Mungu chochote kikilinganishwa na hii hakitakuwa na maana*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
DOWNLOAD APP YETU PLAY STORE 👉📱
SHARE UJUMBE HUU KWA FAMILIA NA MARAFIKI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII HAPA CHINI👇🏾
0 Comments