WILSON SOSSION AJIUZULU

Wilson Sossion amejiuzulu kutoka nafasi aliyokuwa nayo tangu 2013, katika chama cha Kitaifa fha Walimu nchini Kenya (KNUT).

Sossion, ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa, alijiuzulu kutoka nafasi hiyo yenye ushawishi siku moja kabla ya uchaguzi wa Muungano uliopangwa kufanyika Jumamosi katika viwanja vya Ruaraka jijini Nairobi.

Alitoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi akizungukwa na wanafamilia wake wa karibu pamoja na mkewe na watoto. 

Hakuna afisa wa KNUT aliyekuwepo wakati wa kujiuzulu.


No comments