RUNGWE AOMBA SERA YAKE YA UBWABWA ITEKELEZWE

Aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania mwaka 2020 kupitia chama cha ukombozi wa umma(CHAUMMA) Hashimu Rungwe amemshauri rais Samia Suluhu kutekeleza sera yake ya aliyoinadi wakati wa uchaguzi huo wa kugawa chakula bure(Ubwabwa) .Rungwe ametaja maeneo ya kipaumbele yalenge mahospitalini pamoja na mashuleni.

Akizungumza hapo jana june 23,Rungwe amemshauri rais Samia Kuweka ajenda atakayosaidia kuondoa njaa kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini na wanafunzi mashuleni.

Katika kampeni za mwaka 2020 Rungwe aliahidi kutenga pesa kwa ajili ya kugawa ubwabwa bure kwa wananchi endapo wangemchagua.

No comments