TUPIGE STORI: Mimi na Frank tuliamini sana kwenye kushirikiana kama marafiki ili tuje kufanikiwa pamoja, tukiwa shule tulijua biashara ndio sehemu sahihi ya kupata utajiri. Baada ya yale yaliyotokea ( kama ulifuatilia post yangu ya nyuma kuhusu kumpatia pesa Frank tukiwa China)
Kuna shida iliwahi kutokea kati yetu, baada yakuanza kufanikiwa kwenye biashara ya nguo Kariakoo niliamua kuanzisha brand yangu ambayo ndio VUNJABEI na nikafungua duka Sinza sehemu ambayo Frank alikuwa ana duka linaitwa GOOD LOOKING STORE wote tulikuwa tunauza nguo za kiume. Ilifika point biashara zikawa kubwa na tukawa tunashindana sokoni tuligundua hili litatugombanisha.
Tulikaa chini kutafakari na tukaapa hakuna kitu kinaweza kutugombanisha, Tunafanyaje na wote tumeshatengeneza brands kubwa na tunao wateja wengi. This time Frank alisema imefika muda wake kurudi nyuma kama ambavyo mimi niliamua kumpa hela China na kuacha kununua mzigo ili yeye afanikiwe kwanza.
Frank aliamua kufunga duka la GOODLOOKING akatengeneza Brand mpya ya FRANK KNOWS akaamua kuuza nguo za kike ili tuache kushindana na urafiki wetu udumu.
Ilibidi ninunue mzigo wake wote wa nguo za kiume, na akaenda China kufunga mzigo wa viatu vya kike. Tulipambana kwa pamoja kuikuza brand mpya na tukafanikiwa.
Labda hii ndio sababu VUNJABEI imekuwa kubwa zaidi kuliko FRANK KNOWS, na pia ndio Sababu ya Frank mpaka leo kuuza nguo za kike tu.
kipimo cha rafiki yako wa kweli ni kujua ana uwezo gani wa kujitoa ili kuhakikisha unakuwa na furaha na mnapata mafanikio kwa pamoja.
0 Comments