Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameushukuru Umoja wa Nchi za Ulaya kwa kuonyesha nia ya uwekezaji kwenye masuala ya miundombinu ya kijani, kukuza ajira na kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Suala ziama la ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Akiongea na Ujumbe kutoka umoja wa Ulaya kwenye Ofisi ndogo ya Magogoni Jijini Dar-es-salaam Waziri ummy ameupongeza umoja huo kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika Mikoa ya Mwanza, Sumbawanga na Lindi.
Aidha, Waziri Ummy amewashukuru kwa kuonyesha nia ya kuendelea kuwekeza katika miradi mingine ya maendeleo katika Mkoa wa Tanga na kisiwani Pemba.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya Bw, Cedrick Merel ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili na kuhaidi kuwa wataendelea kujenga umoja, ushirikiano, uwazi na uwajibikaji uliotukuka katika suala zima la kuleta maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

0 Comments