• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Habari / UJENZI WA NDEGE NA BARABARA WAKAMILIKA MSALATO

    UJENZI WA NDEGE NA BARABARA WAKAMILIKA MSALATO

    Bisaya Raphael May 09, 2021 Habari
    Fidia ya wananchi wa maeneo wanaopisha ujenzi wa kiwanja cha kimataifa cha Ndege cha Msalato na Barabara ya mzunguko imekamilika na itaanza kutolewa ndani ya muda wa wiki mbili zijazo.

    Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Dr. Leonard Chamuriho wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya uwanja wa ndege Msalato na barabara ya mzunguko.

    “Tumekamilisha taratibu zote za malipo ya fidia ya takribani Tsh 14 bilioni kwa wananchi wote wanaopisha ujenzi wa uwanja wa Ndege Msalato na wanaopisha barabara ya mzunguko,hivyo muda sio mrefu tutawafikia na kuwalipa fedha wananchi wote waliopitiwa na miradi hii mikubwa”Alisema Dr.Chamuriho

    Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu *Mh. Seleman Kakoso* ameitaka Serikali kuhakikisha wananchi wote wanalipwa mapema ili kuruhusu utekekelezaji wa miradi hii mikubwa inayogharimu zaidi ya Trilioni 1 kwa ujumla wake na kuitaka Wizara kuwasimamia wakandarasi vizuri ili miradi yote ikamilike kwa muda uliopangwa.

    Akitoa shukrani zake,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde* ameishukuru Serikali kwa kukamilisha taratibu zote za malipo ya fidia kwa wananchi ambao wamesubiri kwa muda mrefu na kuitaka serikali kuzingatia taratibu zote za kisheria za malipo ya fidia ili kila mwananchi apate haki yake stahili.

    Mbunge Mavunde pia ameishukuru serikali kwa kutenga kiasi cha **Bilioni 16 **ambazo zitajenga vituo vya Afya,Visima virefu vya maji na Gari la kubeba wagonjwa kwa maeneo yote miradi hii ya barabara inapotekelezwa.

    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates