Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imepongezwa kwa kuendeleza utamaduni wake wa kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo mikakati iliyowekwa katika kuimarisha uchumi wa Buluu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa pongezi hizo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China Zhang Zhisheng, aliyefika Ikulu kwa ajili ya Kujitambulisha.
Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa Jamhuri ya Watu wa China ni mdau muhimu wa maendeleo ya Zanzibar kwani imekuwa ikiiunga mkono Zanzibar tokea miaka ya 60 mara baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964.
Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi huyo mdogo wa China anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Zhang Zhisheng kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamani sana juhudi za Serikali ya China katika kuunga mkono miradi mbali mbali ya maendeleo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Jamhuri ya Watu wa China imeweza kuunga mkono sekta mbali mbali za maendeleo hapa Zanzibar ikiwemo afya, elimu, kilimo, viwanda na nyenginezo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar ina furahishwa na juhudi za nchi hiyo za kuendeleza uhusiano na ushirikiano wake katika kuendeleza na kuimarisha sekta za maendeleo.
Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Jamhuri ya Watu wa China katika kuhakikisha sekta za maendeleo zinaimarika sambamba na kuimarisha udugu na urafiki uliopo.
Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi huyo mikakati iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika suala zima la ujenzi wa Bandari mpya ya Mangwapwani na kuwakaribisha wawekezaji pamoja na Kampuni kutoka China kuja kuekeza Zanzibar.

0 Comments