AMKA NA BWANA LEO 9

KESHA LA ASUBUHI
Jumapili 09/05/2021
*NJOZI YA ONYO*
*Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!* *Habakuki 2:15*
Niliota nikiwa ninashangaa kwa nini wewe [ndugu huyu alikuwa anamiliki boti katika pwani ya magharibi] umekaa muda mrefu sana mbali na nyumbani kwako na familia yako, na mbali na nyumba ya Mungu siku ya Sabato, na huonekani kwenye mikutano ya maombi. Wakati huo nilikuwa nimepanda boti yako. Kulikuwa na watu kadhaa wenye uso wa furaha,wakizungumza na kucheka, wakitaniana na kucheza karata. Wewe ulikuwa mmoja wao. Niliona meza zimeandaliwa zikiwa na chakula chenye ubora mzuri ili kukidhi tamaa ya chakula ya watu waliokuwepo. Nilisikia wakiomba pombe.
Nilitazama kwa mshangao niliposikia sauti yako, mwanafunzi wa Kristo, akionekana anatafuta na akitokea kwa haraka, anasema, "Hii hapa ndugu." Mvinyo wa kila aina uliwekwa mbele yao, wakautumia nawe ukanywa pamoja nao.
Kijana ambaye mata nyingi alinifafanulia ndoto zangu, alizungumza nawe akasema, “Unakunywa na kula pamoja na walevi... Nani aliyenunua chupa hizo kwa ajili ya kunywa?” Nawe ukasema, “Nimezinunua mimi, maana nisingepata washirika wa kusafiri pamoja nami kama nisingekidhi hamu yao ya chakula kwa kipengele hiki.”
*Huu ni ushahidi wa kutosha kuwa humpendezi Mungu, na kwamba unajiweka mwenyewe katika uwanja wa majaribu ya Shetani.* Unafanya kafara ya kutisha kwa shauku yako ya ndani ya kupenda kukaa kwenye maji. Ikiwa huu ndio uchaguzi wako, kabla ya kufanya kazi ambayo Mungu angekupatia uifanye, si muda mrefu utazuiwa kuendelea na kazi yako. *Utapoteza ulimwengu huu na ule ujao*
*Baada ya ndoto hii, nilipata nyingine. Niliota tena ulikuwa unatumia tumbaku. Nilidhani kwamba mazoea haya mabaya, yatakaposhindwa, yalikuwa yanafanywa na wewe na kwamba ulikuwa unarudi nyuma, hatua kwa hatua, kwenda gizani, kuuza roho yako kwenye soko la bei nafuu. Lakini sasa nitakuuliza,unapendekeza utafanya nini? Umesimama katika shida kubwa*.
*Nilikuonya, kama ambavyo mama angemwonya kijana wake, kuepuka mambo ambayo yatahatarisha maadili yako, kukuweka katika fedheha kupitia kuendekeza tamaa ya chakula. Ninakupatia kurasa chache hizi kama balozi wa Kristo. Kuwa mwangalifu usije ukapuuza maonyo uliyopewa.*
*UWE NA TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI MPENDWA*
Post a Comment