Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 23

KESHA LA ASUBUHI

JUMAPILI, MEI, 23, 2021
SOMO: KUPATA URITHI 

Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele. 

Yuda 1:7. 



Hali ya mambo katika ulimwengu wetu inatia wasiwasi kweli. Mungu anamwondoa Roho Wake kutoka katika majiji maovu, ambayo yamekuwa majiji kama ya watu wa kale, na kama Sodoma na Gomora. Wakazi wa majiji haya wamepimwa na kujaribiwa. Tumefikia wakati ambapo Mungu anakaribia kuwaadhibu watenda maovu wenye kiburi, ambao wanakataa kushika amri zake na kupuuzia ujumbe wake wa onyo. Yeye anayewavumilia sana watenda maovu humpatia kila mtu fursa ya kumtafuta Yeye na kunyenyekesha mioyo yao mbele Zake. 



Kila mtu ana fursa ya kuja kwa Kristo na akaongolewa, ili aweze kuwaponya. Lakini utafika wakati ambapo hakutakuwa tena na rehema. Majumba ya kifahari, maajabu ya ujuzi wa usanifu majengo, yataharibiwa kufumba na kufumbua, wakati Bwana anapoona kwamba wamiliki wamevuka mipaka ya msamaha. Uharibifu kwa moto wa majengo ya kifahari ambayo yanachukuliwa kuwa yana kinga dhidi ya moto ni kielelezo cha namna ambavyo jengo la kifahari la ulimwengu litakavyoanguka katika uharibifu ndani ya muda mfupi ....



Sura ya ishirini na nne ya Mathayo inatoa kielelezo cha kile ambacho kitaujia ulimwengu. Tunaishi katikati ya taabu za siku za mwisho. Wale ambao wanapotea katika dhambi wanapaswa kuonywa. Bwana anamwita kila mtu ambaye amempatia talanta ya uwezo wa kutenda kama mkono wake wa msaada kwa kutoa fedha zao kwa ajili ya kueneza kazi Yake. Fedha yetu ni hazina ambayo Bwana ametuazima, na inapaswa kuwekezwa katika kazi ya kuupatia ulimwengu ujumbe wa mwisho wa rehema.... 



Yeye ambaye anatazama mambo ya dunia kama mazuri sana, yeye ambaye anatumia maisha yake ili kupata utajiri wa duniani, kwa kweli anafanya uwekezaji mbaya. Atakuwa amechelewa sana kuona kwamba yale ambayo aliyatumainia yanakwenda kuwa mavumbi. Ni kupitia tu kujikana nafsi, kupitia kutoa sadaka utajiri wa duniani, ndipo utajiri wa milele unaweza kupatikana. Ni kupitia mateso mengi ndipo Mkristo anaingia katika ufalme wa mbinguni. Daima atapigana vita vizuri, hataweka silaha yake chini hadi Kristo atakapomwambia apumzike. Ni kupitia tu kwa kumpatia vyote Kristo ndipo ataweza kupata urithi utakaodumu milele zote.



—Letter 90, Mei 23, 1902,, kwa Ndugu 
Johnson, mshiriki wa kawaida.



Post a Comment

0 Comments