AMKA NA BWANA LEO 2
KESHA LA ASUBUHI
JUMAPILI, MEI, 2, 2021
SOMO: KUFANIKIWA KUPITIA KRISTO
Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa.
Matendo 20:32.
Maarifa ya kumjua Bwana yanaongezeka, na yataendelea kuongezeka. Uzushi na ushirikina unaifunika dunia katika mavazi ya gunia ya uasi na ukengeufu. Maandishi na riwaya za kila aina zina sambazwa kama majani ya msimu wa mapukutiko, na akili za wengi zimetekwa na uchafu, mambo yasiyokuwa ya kidini kiasi kwamba hakuna nafasi akilini kwa ajili ya usomaji makini. Neno la Mungu na yale yote ambayo yatamwinua mwanadamu kutoka katika udhalimu yanaachwa bila kujali.
Lakini Neno la Mungu lina ukweli, na wale wote ambao wanaupenda ukweli wa Mungu kwa wakati huu wanafanya kazi yao kwa wakati huu na kwa ajili ya umilele. Wale ambao wanaliweka neno la Mungu akilini na moyoni kwa ubayana kabisa wanakuwa upande wa Mungu na upande wa mbingu. Wasimamia kwa moyo wote na kwa nguvu zote kutetea utakatifu na usafi, ambao utashinda jaribu la muda.
Wale ambao wanatetea makosa kwa neno na kalamu na sauti, na kwa kuwakandamiza wale ambao wameunganishwa na ukweli, wapo upande wa pili, pamoja na mwasi mkuu wa kwanza na watu waovu ambao ni mawakala wake. Neno linasema kuhusu hawa kuwa “watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.” Na wanadamu watafanya kazi kati ya pande hizi mbili hadi mwisho wa wakati.
Uwezo wetu wote ni mali ya Mungu. Ni Wake kwa uumbaji, na kwa ukombozi. Mungu amempatia kila mtu kipimo chake cha uwezo, na anatarajia kila mtu kuutumia katika upande wa ukweli. Hivyo unapaswa uangaze. Mkristo anapaswa kusimama upande wa Bwana bila nia iliyogawanyika. “Sasa inadumu imani, tumaini, upendo.” Imani inapita katika taabu zinazokatisha tamaa, na inashikilia yasiyoonekana, hata Mweza wa yote kwa hiyo haiwezi kutatizika.
Imani, tumaini, na upendo ni dada, na kazi zake hushikamana kikamilifu ili kung’ara katikati ya giza la maadili ya ulimwengu. Watoto na vijana wanapaswa kuelekezwa, wajinga wanapaswa kufundishwa kwa jitihada za ustahimilivu ili kujua ukweli ni nini. Wanapaswa kupewa mstari kwa mstari
—Manuscript 46, Mei 2, 1897, "Mlango wa Neno lako Hutoa Nuru."
Post a Comment