Advertisement

Responsive Advertisement

NITAKWENDA NA BWANA

💼💼💼💼💼💼💼💼💼💼💼💼
*_NITAKWENDA!_*

*_BWANA, NIIMARISHE NAMI NITAKWENDA!_*
👜👜👜👜👜👜👜👜👜👜👜👜
*_[Yoshua 1:9]_*
🎇🎇🎇🎇🎇🎇🎇

*_📖"Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako." (Yoshua 1:9)_*

*_UTANGULIZI:_*
🚥🚥🚥🚥🚥🚥🚥

*👉🏿✍🏽Sisi sote, wakati mmoja au mwingine, tumeshakuwa wahanga wa hofu. Na hofu, amini au usiamini, inaweza kuzuia tusifike lengo ambalo kwako tulikumbwa na Mungu. Kwa sababu ya hofu, baadhi ya Watu wamebadilisha kazi, au wamehamia maeneo mengine ya nchi, wamejifungia ndani ya nyumba zao, au kwenda mafichoni. Ni jambo lisiloweza kuaminika, lakini hofu inaweza kumzuia muuzaji aswese kuuza bidhaa zake; mwanamume anayempenda Mwanamke, akashindwa kumwomba Mwanamke waoane; mtu anayetafuta kazi, akashindwa kumwambia meneja; au mtendaji mkuu, mtu akashindwa kufanya maamuzi ya msingi; na mtu anayetafuta ukweli, akashindwa kutoa maisha yake kwa Mungu.*

*👉🏿✍🏽Marafiki, wapendwa, hofu haibagui Watu na haliangalii umri. Inawapatia Watu dhaifu na wenye nguvu. Inawatesa vijana na wazee, matajiri na masikini. Hata wale ambao huonekana kuwa na kila kitu wanachohitaji; Watu mashuhuri, viongozi, mashujaa, wanakiri kuwa na viwango mbali mbali vya hofu.*

*👉🏿✍🏽Ni nani angefikiri, kwa mfano Kaisari Agusto, mfalme mkuu wa Rumi, alikuwa mwoga wa giza? Au kwamba Napoleon Bonaparte, nguli wa mipango na mikakati ya kivita, alikuwa mwoga wa paka. Kwamba Richard Nixon alikuwa mwoga wa hospitali, na George Washingtoni aliogopa kuzikwa akiwa hai. Lakini, zaidi ya hapo, nani angefikiri kuwa Jonny Depo, mwigizaji nyota wa filamu mashuhuri za miaka ya hivi karibuni, amekiri kuwa anawaigopa wachekeshaji. Ya kwamba Michael Jordani, mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, ana woga wa kupiga mbizi kwenye maji; na kwamba Oprah Winfrey, mmoja wa wanawake wanaotambulika sana ulimwenguni, anaogopa kufanya uamuzi.*

*_UFAFANUZI:_*
🚥🚥🚥🚥🚥🚥🚥

*👉🏿✍🏽Ni jambo linalosisimua kuwa Biblia, kitabu ambacho ndicho kitabu hasa, kinachozungumzia kwa kina mada ya hofu. Kwa mujibu wa wasomi, istilah _"usiogope"_ inatokea karibu mara 365 katika Maandiko, hivyo kuifanya kuwa amri ambayo umerudiwa mara nyingi kuliko amri zingine zote. Kwa upande mwingine, neno _"ogopa"_ hutokea zaidi ya mara 200, wakati, _"hofu"_ au _"tishio"_ zaidi ya mara 100 kila moja. Na ili usifikiri kuwa mashuka wa kwenye Biblia hawakuwa na hofu, Maandiko yanasema kuwa zaidi ya Watu 200 waliogopa._Itaendelea>>>_*

Post a Comment

0 Comments