SIYO KILA MAJI YANAFAA KWA UBATIZO!
Haleluya!
Kwa jina la Yesu ninapenda leo tujifunze kuhusu maji yanayofaa kwa ubatizo. Kwakuwa ni kweli siyo kila maji yanafaa kwa ubatizo.
Tuanze na Yohana 3:22-23"... walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi...akabatiza.Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni...kwasababu huko kulikuwa na maji TELE..."
Haleluya!
Katika mstari wa 22 tunaona bwana Yesu na wanafunzi wake wanasafiri mpaka nchi ya Uyahudi ili kutafuta maji ya kubatiza watu. Hii haina maana kwamba nazareth walikuwa hawaogi au hawanywi maji au hawafugi.. Bila shaka watu wa Galilaya walikuwa wanakunywa maji ,hebu soma Yohana 2:7"... Jalizeni mabalasi MAJI..."
Unaona kabisa kuwa Galilaya kulikuwa na maji,lakini maji hayo hayakufaa kwa UBATIZO ndiyo maana Yesu alisafiri mpaka UYAHUDI ili kutafuta maji ya kubatizia watu... Siyo kila maji yanafaa kwa ubatizo.
Sote tunajua kuwa Yohana mbatizaji alikuwa anabatiza katika mto Yordani,na Yesu naye alitumia mto huohuo kubatiza,japo yeye hakubatiza bali wanafunzi wake >Yn.4:2.
Kwahiyo maji yanayofaa kwa ubatizo yanatakiwa yawe:
1. Yanatiririka hii ni ishara ya kuwa yako hai,lakini yaliyosimama tu,yanakuwa siyo hai.
2.Ya asili yasiwe ya kusombelea au yasiwe ya asili lakini hayatiririka.
3.Yanatokana na chemichemi.
4. Mengi au tele yakutosha mtu kuzama au kuzikwa mwili mzima.
Zekaria alutabiri hizi,Zekaria 13:1" katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi,na wenyeji wa Yerusalemu,watafunguliwa chemichemi kwa dhambi na kwa unajisi."
Utabiri huu ulitimia baada ya Yesu,ni utabiri juu ya ubatizo katika maji hai na ya asili( chemichemi).
Ubatizo ni kuoshwa siyo kunwagiwa maji.1kor.6:11"..., lakini mlioshwa,..." Isaya.1:16" jiosheni..."
Ubatizo wa kutumia maji haya na kunyinyizia watu haufai.
Maji yenye sifa hizi yanatokana na:
1.ziwa
2.bahari
3.mto
4. Chemichemi ( katika chemichemi ya maji ni vizuri kuchimba shimo kubwa na kuyakusanya maji ili watu watoshe kuzamishwa humo)
Barikiweni.By Apostle Mugongo,0753833236
0 Comments