Gwambina FC wanaruhusu kupigwa nyumbani na Mnyama Simba SC, mchezo umemalizika kwa Simba kuondoka na ushindi wa bao 1 - 0, goli lililogungwa kwa ufundi wa hali ya juu na uimara wake kutoka kwa Muhamed Hussein "ZIMBWE JUNIOR " maarufu pia kwa jina la "TSHABALALA dakika ya 29 tu ilimtosha yeye kupachika bao hilo.
Hivyo Simba SC kwa sasa anaongoza Ligi akiwa na Points 58, huku akiwa amecheza mechi 24, huku watani wao Young Africans YANGA SC, wakifatia nafasi ya pili wakiwa na points 57, wakiwa wamecheza mechi 26.
Hivyo mnyama Simba SC badi ana viporo viwili mkononi.
0 Comments