Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 25

KESHA LA ASUBUHI

Jumapili 25/04/2021

*DAIMA MBELE*

*Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.* *Yohana 16:7, 8*

Serikali ya Shetani hudhibitiwa na kutawaliwa kwa wakala wenye nguvu wa Roho Mtakatifu. Ni Roho Mtakatifu anayesadikisha dhambi, na kuiondoa nafsini kwa maridhiano na wakala wa kibinadamu. Mawazo hutiishwa chini ya sheria mpya na sheria hiyo ni sheria ya uhuru ya kifalme. *Yesu alikuja kuzivunja pingu za utumwa wa dhambi katika nafsi;* kwani dhambi huweza kushinda tu pale uhuru wa nafsi unapofishwa. 

*Yesu alifika hadi kwenye kina kabisa cha huzuni na taabu ya mwanadamu, na upendo wake unamvuta mwanadamu Kwake*. Kupitia uwakala wa Rohc Mtakatifu anayainua mawazo juu kutoka katika uharibifu wake na kuyaimarisha katika ukweli wa milele. Kupitia stahili za Kristo mwanadamu anakuwa na uwezo wa kutendea kazi uwezo mkuu wa nafsi yake na kuiondoa dhambi nafsini mwake.

Tunavyotembea katika amri za Mungu, tunafuata njia ambayo Bwana mlipa fidia yetu aliipata. Waaminifu katika zama zote walitembea katika njia hii na waliangaza kama nuru katika ulimwengu. Katika zama hizi, nuru iliyopitishwa kutoka kwao imekuwa ikiangaza kwa mwangaza ulioongezeka njiani mwa wale wanaotembea gizani. 

Baadhi wameupokea ukweli, wakauamini na kuutii. *Nuru ya ujumbe wa malaika wa tatu imepenya katika akili nyingi) zilizotiwa giza. Nuru ya hekima, wema, rehema na upendo wa Mungu imekuwa ikiangaza kupitia Neno Lake. Hatupo katika eneo ambalo wazazi wetu walikuwa. *Nuru kuu inaendelea kuangaza katika siku hizi za mwisho*. Hatuwezi kukubaliwa na Mungu; hatuwezi kumheshimu kwa kutoa huduma ile ile, na kwa kuzifanya kazi zilezile ambazo wazazi wetu walizifanya. 

*Ili kuhesabiwa kutokuwa na hatia mbele za Mungu, ni lazima tuwe waaminifu wakati wa zamu yetu katika kufuata na kutii nuru yetu kama wao walivyokuwa waaminifu kufuata na kutii nuru ambayo iliwaangazia. Kwa kila mshiriki wa kanisa Lake, Baba yetu wa mbinguni anahitaji, imani na matunda kulingana na neema na nuru waliyopewa. Mungu hatakubali pungufu ya hapo. Kila nafsi ni lazima ijiweke mahali ambapo nuru itamwangazia. Anatakiwa kuthamini kila mwali, ili apate kung’arisha na kubariki roho za wengine kwa miali iliyotumwa kutoka mbinguni.*

*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*

Post a Comment

0 Comments