Kuanzisha mahusiano kupitia mitandao ya kijamii

Amekutext Inbox WhatsApp📥

Ukamuuliza we nani?🙂

Akakujibu jina👶🏽

Ukamuuliza umepata wapi namba yangu?😒

Akakujibu, nimepata kwenye lile group tupo wote😊

Ukachukulia poa tu😏

Ulivyoingia fb ukakuta amekutumia urafiki Friend Request facebook👤

Ukam Confirm

Ukaingia katika Timeline yake.

Ukaangalia picha zake👱🏽

Anaendesha Range🚘

Anaonekana ni jamaa mwenye uwezo🤑

Amekutumia text inbox📩

Umemjibu📤

Amekuomba muonane👫

Mkapanga kuonana😄

Ukamwambia atume nauri.

Bila kuchelewa sms ya TIGOPESA ikalindima kwenye simu yako.

200,000 ni nauri umetumiwa ingawa unapotokea na unakokwenda haizidi 70,000.

Ukajikwatua mwenyewe😋

Ukajipulizia na marashi ya kunukia vyema🌹

Ukaweka na make-up na weave mpya.💄👠

Ukapanda usafiri.

Ukafika.

Akakuchukua kwa ajili ya lunch🍛🍨 kwa hotel🏩

Akakuagizia na soft drinks🍹🍸

Mkawa na muda mzuri pamoja😄😅

Akakushika mkono👌🏾

Akakufanya uwe unacheka😆 muda wote kwa vituko vyake

Ukampenda😍

Ikawa kama umemjua kwa miaka😊

Akakuchukua kwenda kwake🏡

Akaweka mazingira ya wewe kujisikia upo kwako kwa kukuruhusu ulale kitandani kwake🛌

Akakubusu kimahaba😘

Ukapenda jinsi alivyo romantic, nguvu na ujasiri🤓

Ukajisikia secure ukiwa nae😀

Ukajua kuwa unachoenda kufanya sio sahihi lakini ukajisikia poa tu🙂

Ukamwambia atumie kinga, akakuambia it's too late.😎

Ukamkubalia na hukutaka kumsumbua.😟

Akakuambia anakupenda na hukusita kumwambia unampenda pia.😉😘

Baada ya kumaliza akafungua friji na kukunywesha maji ya kunywa. Ukajihisi hapa mume nimepata🤗

Ukajihisi ni mwanamke special💁🏽

Atakuwa ndio yeye uliyekuwa ukimuota siku zote.💃🏽

Ukavua nguo👙

Mkafanya💏

Ukavaa nguo.👗

Akakuchukua mpaka sehemu zinakopaki taxi🚗

Akakubusu katika shavu.😘😆

Nimekuwa na muda mzuri na wewe akakueleza.💁🏽💁🏽‍♂

Akakupa Tsh 300,000💵💴💷💷. 

Ukatabasamu😊 na kumwambia nitakuona kesho.

Akabaki kimya.🤐 Taxi uliyopanda ikaondoka.🚖

Ndani ya taxi hukuacha kutabasamu😊

Ukafika nyumbani kwenu na kumwandikia text watsapp kwamba umefika salama.😁

Yupo online lakini hakujibu text yako🤔

Ukaamua kumtext tena, hakujibu!🤔

Dakika chache baadae humuoni WhatsApp unaona kivuli tu. AMEKUBLOCK!!🌚

Siku, wiki, miezi ikapita ukaanza kujisikia homa homa😪, mchovu😣, uzito umepungua na utando mdomoni😤

Ukaenda kituo cha afya🏘

Ukapima🌡💉

Nusu saa baadae daktari anaingia.👳🏽

Pole sana dada yangu daktari anakuambia.😟

Una maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ni mjamzito vile vile😔.

Mimba, HIV+????😳

HOW??👀

Hauelewi😖

Inakuumiza sana😩, hauamini.😨

Unaenda nyumbani.🏠

Ukiwa na hofu kubwa.😰

Unaona kifo hichi hapa👁

Unatazama angani🙄, na unauona mwisho wako huu hapa. Unajuta kumuamini mtu kirahisi hivyo.😟

WASICHANA WANGU, MSIWE KAMA HUYU, ISHI VIZURI, ACHA KUTAMANI MATERIAL THINGS. KUWA MWANAMKE AMBAE UNGEPENDA BINTI YAKO AJE KUWA HIVYO.

ISHI MAISHA YANAYOMPENDEZA MWENYEZI MUNGU PEKEE NA SIO BINADAMU.

SIJAKATAZA MSIAMINI WACHUMBA WA FACEBOOK na WHATSAPP ILA MUHIMU MTANGULIZE MWENYEZI .

✍️
Patrick Patrick CHALAMILA
(MSD third year)

No comments