WENYE NYUMBA ZA TOPE MBEYA MJINI KUHAMISHWA

WENYE NYUMBA ZA TOPE MBEYA MJINI KUHAMISHWA

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya imeagizwà kuwahamisha watu ambao nyumba zao hazipo kwenye mpangilio wa mipango miji na kuwapatia viwanja vingine pembezoni mwa mji.

Agizo hilo lilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja wakati akizungumza na Madiwani pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo katika mkutano wa Baraza la Madiwani.

Mtunguja alisema jiji la Mbeya bado haliendani na hadhi ya kuitwa jiji kutokana na hali ilivyo kwenye mpangilio wa makazi.

Niaibu sana kuona mpaka leo hii eti ukipita katikati ya mji kuna nyumba za tope, kila Nyumba na langi yake, halafu jiji mnawatalaam wa mipangomiji ambao wanaweza kushauri namna bora ya kupanga makazi yetu na tukawa na jiji linalo vutia kama ilivyo majiji mengine, alisema.
#BinagoUPDATES

No comments