sikia Sauti Hii
*_JE, UMEISIKIA SAUTI HII?_*
🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊🔊
*_"Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya." (ISAYA 1:16-20_*
*_"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi." (Matayo 11:28-30)_*
*_ASIYESIKIA LA MUNGU ATAVUNJIKA SHINGO._*
*_"Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa." (Mithili 29:1)_*
*_MUNGU ATUPE KUSIKIA SAUTI YA HOJA YA MSAMAHA. NEEMA YAKO ITUBADILISHE, UTUSAFISHE DHAMBI ZETU SAWASAWA NA AHADI YAKO BWANA, LAKINI SI KWA MAPENZI YA MWANADAMU, BALI MAPENZI YAKO BABA YATIMIZWE, KATIKA JINA LA YESU KRISTO BWANA MWOKOZI WETU. AMINA._*
🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Post a Comment