kucheza katika ibada ni Dhambi
😕😕😕 *JE, NI HALALI KUCHEZA KANISANI WAKATI WA IBADA??* 😕😕😕
.
.
Kumbuka kuimba na kucheza ni vitu viwili tofauti unaweza kuimba bila kucheza au kucheza bila kuimba au kuimba na kucheza
.
.
.
Wajua kuwa kunanyimbo ni kelele mbele za MUNGU na sisi wanadamu tunadhani ni za kumsifu MUNGU??? Amosi 5:22,23(naam ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za amani na za wanyama walionona niondoleeni kelele za nyimbo zenu kwa maana sitaki kusikia sauti za vinanda vyenu.
.
.
.
Kwa akili yetu wanadam tunadhani kila nyimbo inayo taja jina la MUNGU au Yesu ni nzuri kwake lakini MUNGU wetu anatwambia zingine ni chukizo kwake
Je, uimbaji kama huu unamtukuza MUNGU kweli?? 🤔🤔
.
Je, nyimbo chukizo kwake zikoje???
.
Amosi 6:5-7 (ninyi mnaoimba nyimbo za upuuzi pamoja na sauti ya vinanda ................... Kama vile Daudi ................... Basi kwa ajili ya hayo sasa watakao kwenda utumwani na kelele za MACHEZO za hao walio jinyoosha zitakoma.
*NB*
Kumbuka zaburi imeandikwa na daudi
.
Yatupasa tujifunze kupambanua tofauti iliyo kati ya vitu vitakatifu na vitu vya siku zote na kufundishana kupambanua kati ya yaliyo machafu na yaliyo masafi ezekieli 44:23
.
Jambo la kuimba ni jema mbele ya MUNGU wetu basi (maana MUNGU ndiye mfalme wa dunia yote, IMBENI KWA AKILI ) zaburi 47:7 pia 1 koritho 14:15
.
Tangu mwanzo waliimbaje kwa akili???????
.
2 nyakati 5:12 (tena walawi waimbaji, wote pia na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, #WAMESIMAMA upande wa mashariki wa madhabahu na pamoja na makuhani mia na ishirini wapiga panda)
.
Tangu mwanzo waliimba kwa kusimama tena kwa kicho na heshima kuu bila kelele wakimtukuza MUNGU MUUMBAJI WETU MTAKATIFU WA WATAKATIFU CHEMICHEMI YA WATAKATIFU WOTE
.
Je, tukifika mbinguni tutaimbaje??????
.
Ufunuo 7:9-12 pia ufunuo 15:2,3(tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyo changamana na moto na wale wenye kushinda watokao kwa yule mnyama na sanamu yake na kwa hesabu ya jina lake walikuwa #WAMESIMAMAAA kando kando ya hiyo bahari ya kioo wenye vinubi vya MUNGU nao WAIMBA WIMBO WA MUSA mtumwa wa MUNGU NA WA MWANA KONDOO ...........................
basi tukifika mbinguni (itakuwa sabato hata sabato mwezi mpya hata mwezi mpya tutafanya ibada mbele za MUNGU wetu na kuimba bila kucheza isaya 66:
Lakini baada ya sabato na mwezi mpya tutakuwa tunacheza cheza si mbele ya MUNGU bali nje ya mji malaki 4:1-3
Kwa hiyo kwa kuwa (BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu dunia yote na inyamaze kimya mbele zake) habakuki 2:20
.
Sasa basi wakristo tukiwa ibadani tunapaswa kuwa watulivu wala hatuchezi wala kupigapiga kelele bali tukifanya ibada kwa kicho na heshima kuu bila kunengua nengua na kucheza utafikili disko na nyimbo zisizofaa zenye midundo utafikili ni *yamoto bendi* (uimbaji wa sasa hauna tofauti na uimbaji wa watu wa mataifa) sijui kwanini tunamchukiza MUNGU WETU kwa uimbaji mbaya wa namna hii??? 😢😢
.
Ila sehemu zingine kama mbele ya mumeo au mkeo kucheza waweza cheza maana isaka alicheza na mke wake mwanzo 26:8 au kufurahia kitu furani mfano kumshinda adui zenu au mtihani au nk kutoka 15:20 au sherehe 1 samweli 18:6,7 au yeremia 31:13 zekalia 8:5
.
Alie na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa ufunuo 3:22
.
MUNGU WETU NI WA UTARATIBU basi tutii na kuyafuata maandiko matakatifu na tumuabudu kwa kicho na heshima kuu sana
.
Isaya 1:19-20
[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
[20]bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya. 🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏Ameni
Toa maoni yako hapa chini kama yapo,tujifunze wote🙏🔥
Post a Comment